GET /api/v0.1/hansard/entries/1197485/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1197485,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1197485/?format=api",
"text_counter": 27,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bw. Naibu wa Spika, naunga mkono Taarifa hiyo ya mwanamasumbwi aliyebobea sana. Wanamichezo wetu husifika tu wakati wanafanya vizuri. Kwa mfano, Waruinge alisifika sana katika mchezo wa masumbwi na kupokea nishani tele. Jambo la kuvunja moyo ni kwamba hawakumbukwi hata baada ya wao kufanya Kenya kujulikana kote ulimwenguni. Mara nyingi, utakuta wanamichezo wanaishi maisha ya shida ilhali walifanya nchi yetu kujulikana kila mahali."
}