GET /api/v0.1/hansard/entries/1197487/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1197487,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1197487/?format=api",
    "text_counter": 29,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Sio Waruinge pekee yake. Kuna wanamasumbwi wengine kama vile Conjestina Achieng’ ambaye alifanya Kenya ikajulikana ulimwenguni, lakini hatuwakumbuki licha ya sifa tuletea. Taarifa hii inafaa kushughulikiwa na kamati huzika ili kuhakikisha kuwa kama si wachezaji wenyewe, basi familia zao ambazo hufanya Kenya kujulikana ulimwenguni zinafaa kufidiwa. Inasikitisha kuwa licha ya wao kufanya Kenya ijulikane kila mahali, familia zao zinabaki katika hali ya uchochole. Bw. Naibu Spika, jambo hili lichukuliwe kwa umakini sana. Nampongeza Sen. Cherarkey kwa sababu Taarifa hii inahusu wanyonge na amekuwa akiongea mambo yao hapa. Nashukuru na kumuunga mkono."
}