GET /api/v0.1/hansard/entries/1197677/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1197677,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1197677/?format=api",
    "text_counter": 219,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu Nambari 51(1), kuomba Taarifa kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Usalama wa Taifa, Ulinzi na Uhusiano wa Kimataifa kuhusu kuvunjiliwa mbali kwa Kitengo cha Upelelezi wa Jinai. Katika taarifa hiyo, Kamati iangazie yafuatayo- (1)Sababu zilizopelekea kuvunjwa kwa Kitengo hicho kwa ghafla; (2)Idadi ya watu waliouliwa au kukamatwa na kitengo hicho, na iwapo kuna wananchi wowote ambao walikamatwa na kuwekwa kizuizini bila kupelekwa Mahakamani; (3)Iwapo Serikali itawalipa ridhaa wale wote walioshikwa bila ya makosa ama bila kupelekwa Mahakamani, na; (5)Hatua zitakazochukuliwa kwa maafisa waliohusika na uhalifu huu, ili dhambi na hujuma kama hizi zisitokee nchini kwa siku za usoni."
}