GET /api/v0.1/hansard/entries/1197679/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1197679,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1197679/?format=api",
    "text_counter": 221,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Naibu wa Spika, kwa kuongezea ni kwamba, hivi majuzi kulikuwa na taarifa kwamba mhe. Rais amevunjilia mbali kile kitengo cha Upelelezi wa Jinai kinachoitwa Special Service Unit (SSU). Tukiangalia kutoka Mwaka wa 2013 hadi 2022, Zaidi ya watu 2,000 wameweza kupotezwa na wengine kuweza kuuawa kinyama na vitengo vya usalama. Hawa wote wameuawa bila kupelekwa mahakamani. Hivyo basi, hawakupewa nafasi ya kujitetea kwa yale makosa ambayo walituhumiwa kufanya. Nikizungumzia Mombasa, waliuliwa Sheikh Abud Rogo, marehemu makaburi na wengine wengi. Wote waliouliwa kinyama na polisi bila sababu zote za kisheria."
}