GET /api/v0.1/hansard/entries/1197693/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1197693,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1197693/?format=api",
"text_counter": 235,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Thank you, Mr. Deputy Speaker, Sir. Ninamshukuru Sen. Thang’wa kwa kuelewa ya kwamba bendera iliyoko pale sio ya Kaunti yake. Kwa hivyo, anafanya kazi yake ya oversight na kuangalia kila mahali. Ninakumbuka nilipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ugatuzi, nilikuwa nikiangalia mambo kwa kindani. Bw. Naibu wa Spika, kumekuwa na shida katika Kaunti yako kati ya Gavana na madiwani. Gavana Mwangaza alipoanza kutoa hotuba yake, madiwani wote walitoka nje mara moja. Sisi kama Maseneta, kazi yetu ni kuangalia vile kaunti zetu zinaendelea. Bw. Naibu wa Spika, huenda ikuwe vigumu wewe kusema, lakini nimeona niseme kwa sababu jambo hilo silo nzuri. Kwa hivyo, ningeomba Gavana pamoja na madiwani wa Kaunti ya Meru, wakae chini na waongee. Siku ni chache sana. Hata mwaka haujaisha kutoka uchaguzi ufanyike. Ni vizuri wakae chini, waongee na wakubaliane ili watatue hayo matatizo."
}