GET /api/v0.1/hansard/entries/1197749/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1197749,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1197749/?format=api",
    "text_counter": 291,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Bw. Naibu wa Spika, ndio niweze kuweka mambo haya bayana, ni vyema niseme ya kwamba nilikuwa diwani wa sehemu inayoitwa Mutara. Pia nilikuwa Mwenyekiti wa Kaunti ya Laikipia. Kwa hivyo, Sen. Olekina aelewe hayo. Naona Sen. Madzayo anababaika. Bw. Naibu wa Spika, nataka kwanza kuunga mkono taarifa iliyotolewa kuhusu janga la njaa. Ni ukweli kuwa kuna janga la njaa. Ukitembea sehemu nyingi ya Jamhuri ya Kenya kama Kaunti ya Laikipia, Narok, Lamu na sehemu nyinginezo, utaona ya kwamba tuko na hili janga la njaa. Kwa hivyo, tungeomba Serikali inunue mifugo kutoka kwa wale walio na wanyama, hasa katika sehemu za Mutara na Moran, kwa sababu hata wao wana ile shida ya wanyama kufa. Serikali inaweza kuwapa nyama watu ambao wamekumbwa na janga la njaa. Bw. Naibu wa Spika, naunga mkono Taarifa hiyo na ni vyema niseme ya kwamba janga la njaa haliko katika Kaunti ya Laikipia pekee. Ukitembea sehemu za Kaunti ya Kitui, kuna watu wanaoishi katika hali ya uchochole. Serikali inapaswa ichukulie jambo hili kwa makini na waweze kusaidia wakulima wetu. Kitengo kimoja katika Serikai yetu ya Kenya Kwanza ni mambo ya kupigana na njaa na najua tumejitolea maanga na tutafanya hivo. Bw. Naibu Spika, jambo la pili ni kuhusu madiwani. Madiwani ni viongozi kama wale wengine. Ukitembea katika sehemu zetu za Kenya, utapata waliokuwa Wabunge wanapewa ridhaa. Maafisa wengine wa Serikali pia wanapewa ridhaa."
}