GET /api/v0.1/hansard/entries/1197751/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1197751,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1197751/?format=api",
"text_counter": 293,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Madiwani waliohudumia nchi ya Kenya, kama vile Sen. Wambua alivyosema, walikuwa zaidi ya 12,000. Lakini tunapoongea hivi sasa, 9,000 ndio waliobaki na wanaishi maisha ya umaskini na ufukara. Ukitembea sehemu zingine, utawapata wameajiriwa kuchunga mifugo au kazi za kuosha nguo. Tunaomba waangaliwe na wafidiwe. Kama vile, Sen. Wambua, alivyosema, wajumuishwe na wazee wengine wakati wanapewa tiba ya NHIF. Ni vizuri niwaambie Masenata walioko hapa kwamba Mhe. Najib Balala, Mhe. Maina Kamanda na pia Sen. (Dr.) Oburu kutoka Siaya walikuwa madiwani."
}