GET /api/v0.1/hansard/entries/1197778/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1197778,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1197778/?format=api",
    "text_counter": 320,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Sen. Olekina alivyosema, kuwa akimbie kwa marafiki zake kule Bunge la Kitaifa kuwatongoza. Tuko na uwezo katika Kamati ya Leba na Maslahi ya Jamii, kuchukua hatua na kusema kuwa ile pesa ya ridhaaa iliyopitishwa ilipwe. Tuko na Mawaziri wapya waliochaguliwa. Tuna imani kuwa yule Waziri wa Leba hataanguka ukaguzi. Ripoti yake ikiwa safi, ataanza kazi haraka iwezekanavyo. Kuna umuhumu wa kuwapatia hawa madiwani wazee walioanzisha serikali za ugatuzi heshima yao. Bila hao hatungeweza kusimama hapa leo hii na kusema kuwa tunataka seriakali za ugatuzi ziendelee vipi. Wao ndio waliotengeneza Serikali za mashinani ndipo sisi tukachukua kutoka kwao tukasema hizo zitakuwa serikali za ugatuzi. Ni lazima tuwaheshimu. Nampa Kongole Seneta wa Kitui, Seneta mchapakazi, Sen. Wambua, kwa Taarifa aliyoileta."
}