GET /api/v0.1/hansard/entries/1198118/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1198118,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1198118/?format=api",
"text_counter": 173,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika. Kwanza, ninampa kongole dada yangu, Sen. Kibwana, kwa kuleta taarifa hiyo. Pili, ninakubaliana na yote aliyosema. Tuliona picha za huyo mtoto katika magazeti, akiwa na uma jembe kichwani mwake. Ninaunga mkono ya kwamba madaktari walichelewa kumhudumia yule mtoto. Hata hivyo, hilo silo jambo pekee. Kulikuwa na ukosefu wa madaktari katika hospitali za kaunti lakini wakaandikwa lakini sasa inaonekana wamezembea kazini. Miezi miwili ama mitatu iliyopita, Bunge la Kitaifa lilimpoteza Mhe. William Kamoti, ambaye alipata ajali katika barabara ya Mombasa-Kilifi. Alipelekwa hospitali saa mbili usiku lakini madaktari walikuja saa nane. Hiyo ni baada ya masaa sita. Hospitali ya Kilifi iko karibu sana na pale ambapo ajali hiyo ilitokea. Ni kama kilomita mbili ama tatu. Wasamaria wema walimchukua Mhe. haraka na kumpeleka hiyo Hospitali ya Wilaya ya Kilifi. Iwapo daktari angefika mapema, labda baada ya nusu saa hivi au dakika kumi na tano, tuko na imani Mhe. Kamoti asingepoteza maisha yake. Mhe. Kamoti alikuwa wakili mkubwa huko pwani na Kenya nzima na pia alikuwa mwakilishi wa eneo Bunge la Rabai."
}