GET /api/v0.1/hansard/entries/1198441/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1198441,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1198441/?format=api",
    "text_counter": 78,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, asante kwa kunipa fursa hii kuchangia ardhihali ambayo imeletwa Bungeni na Seneta wa Homa Bay, Sen. M. Kajwang’. Jambo ambalo Sen. M. Kajwang’ amezungumzia katika ardhihali hii ni muhimu sana kwa sababu usafiri wa majini hutumika hususan katika Jiji la Mombasa na Mji wa Lamu ambako kuna visiwa vingi. Tangu huduma za ferry zianzishwe kule Mombasa, hazijawahi kupanuliwa kwa njia yoyote. Ijapokuwa ferry zimeongezeka, hakujakuwa na upanuzi wowote wa huduma za ferry katika Kaunti ya Mombasa. Labda kina Sen. M. Kajwang’ wanalia ngoa kwamba hawana ferry . Kwetu sisi, huduma zinazotolewa pale ni duni sana kwa sababu Serikali haijawekeza katika huduma zile. Bi. Spika wa Muda, itakumbukwa kwamba KFS iliundwa baada ya ajali ya ferry ambayo ilitokea mwaka wa 1994 ambapo karibu watu 250 walipoteza maisha Ferry ya Mtongwe ilipozama. Baada ya muda, huduma zilidorora kwa sababu Serikali haijakuwa ikiwekeza kule. Mpaka wananchi wapige kelele ndio ferry ziongezwe. Swala hili si la Serikali kuu pekee yake. Serikali za kaunti pia zinafaa ziekeze katika mfumo huo wa usafiri,"
}