GET /api/v0.1/hansard/entries/1198500/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1198500,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1198500/?format=api",
"text_counter": 137,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Mambo ya usalama na ufugaji yamekuwa yakiandamana. Ni vuzuri ijulikane wazi kuwa kazi kuu ya Serikali ni kulinda maisha na mali ya wananchi. Jambo ambalo limekuwa likitendeka katika Kaunti ya Laikipia ni kuwa wafugaji wanalisha wanyama wao kwenye mashamba ya watu, na kusema kuwa wanawalisha nyasi sio mchanga. Mchanga ni yako lakini mimea ni ya wanyama. Ni vizuri ijulikane kuwa mashamba yana wenyewe. Hakuna mtu anayesema kuwa mfugaji hafai kuwa na mifugo yake. Anafaa kufuga mifugo inayoweza kutoshelezwa na shamba lake. Mkulima pia ana haki yake, kwa sababu anategemea mimea ile. Wewe unayetegemea mifugo, iweke mahali inapotoshea. Tunafaa kuheshimiana. Mkulima na mimea, na mfugaji na mifugo yake, Kenya ni yetu sote tunafaa kuishi kama kitu kimoja. Mimea haipandwi kwa shamba la mfugaji. Naunga mkono Taarifa iliyoletwa na Sen. Wambua, ya kwamba wale ngamia wachungwe katika mashamba yao. Wafugaji wapewe haki yao kikatiba na kisheria kwa kuwa wanaishi katika nchi hii yetu."
}