GET /api/v0.1/hansard/entries/1198509/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1198509,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1198509/?format=api",
    "text_counter": 146,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Bi Spika wa Muda, katika Mjadala unaoletwa katika hili Bunge, singependa kukueleza utakavyofanya. Najua kazi unafanya kisawasawa lakini haki na utendaji kazi lazima uende pamoja. Upande huu una haki ya kuchangia. Nashangaa kuwa unaelekeza pande moja waongee na upande huu huapewi nafasi. Sitaki kukosoa uamuzi uliofanya, lakini kwa wakati mwingine tukipata fursa kama hiyo ingekuwa bora utoe nafasi upande huu ili usikize maoni yao sawasawa. Isiwe kuegemea upande mmoja na kuwacha mwingine."
}