GET /api/v0.1/hansard/entries/1198642/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1198642,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1198642/?format=api",
    "text_counter": 279,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, katika hiyo Kamati, tumesomewa majina. Katika hayo majina, sisi tumeonelea ya kwamba wote ambao wamechaguliwa wanafaa kabisa katika zile nyadhfa. Wote waliochaguliwa pia wanao uwezo wa kutuwakislisha sisi kama Bunge katika Kamati ndogo itakayochunguza. Kwa hivyo, nina imani na yule aliyechaguliwa kama Mwenyekiti. Ni wakili aliyebobea, ndugu yetu Sen. Maanzo, Seneta wa Kaunti ya Makueni, na anayo tajriba ya kuifanya ile kazi. Vile vile, amekuwa akijihusisha sana na Korti la Afrika Mashariki. Amekuwa huko na amekuwa akifanya hizi kazi na zingine zinazohusiana na Bunge letu la Afrika Mashariki. Katika ile hali, tumeona yeye ana tajriba ya juu sana. Anaweza kukadria na kufikia kile kiwango Bi. Spika wa Muda, tunawatakia kila la heri katika kazi hii ambayo watatuwakilisha sisi kama Bunge la Seneti. Tuna imani ya kwamba kazi wanaijua na wataifanya. Niko na imani na Maseneta hawa wote ambao tumeweza kuwaweka hapo. Naunga mkono yote aliyosema ndugu yangu Kiongozi Wa Walio Wengi."
}