GET /api/v0.1/hansard/entries/1199051/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1199051,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1199051/?format=api",
"text_counter": 277,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
"speaker": null,
"content": "Ningetaka kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana wananchi wa Nakuru kwa kunipatia nafasi mara ya tatu kuja hapa katika Bunge la Taifa ili niwakilishe mambo yao. Tunajua kiti chetu cha Mama Kaunti kinajulikana. Lakini kusema kweli, sisi huchaguliwa na kaunti yote na inafaa tuhudumie watu wote hasa vijana, wamama na walemavu ama wasiojiweza kimaisha. Nataka kushukuru watu kutoka maeneo Bunge ya Nakuru kama vile Kuresoi South, Kuresoi North, Molo, Njoro, Rongai, Nakuru Town West, Nakuru Town East, Bahati, Subukia, Gilgil mpaka Naivasha. Nawaombea Mungu awabariki sana. Nawaahidi kwamba tutafanya kazi pamoja kwa njia ya amani."
}