GET /api/v0.1/hansard/entries/1199144/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1199144,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1199144/?format=api",
"text_counter": 370,
"type": "speech",
"speaker_name": "Shinyalu Constituency, ANC",
"speaker_title": "Hon. Fred Ikana",
"speaker": null,
"content": "Kwanza kabisa, katika sehemu yetu ya Shinyalu, tuko na changamoto kubwa ya miundo msingi. Unafahamu kwamba katika nchi hii yetu ya Kenya, ni miji tu mikubwa ambayo iko na barabara nzuri na safi. Huko Shinyalu hatuna barabara ya rami. Nataka nitilie mkazo barabara ya kutoka pale kiwanja cha ndege hadi kuingia pale Rondo - Ileho hadi Chepsonoi. Kando na mambo ya barabara, nitakuwa natilia mkazo mambo ya masomo ili turekebishe na kukarabati madarasa yetu. Pia kuhakikisha kwamba wanafunzi wetu wanasoma katika shule ambazo ni nadhifu."
}