GET /api/v0.1/hansard/entries/1199419/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1199419,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1199419/?format=api",
    "text_counter": 209,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bwana Naibu Spika. Kwanza ningetaka kuafiki Hoja na kusema kuwa nawaunga mkono Maseneta wanne waliochaguliwa kwenye orodha kwa kuwa iko sawa kabisa. Ningetaka pia kutaja kuwa kutoka Bunge hili la Seneti lianzishwe 2013, hakuna shida tumepata katika kuchagua Maseneta hawa wanne wa Jopol la Spika kwa sababu tumekuwa tunaachia jukumu hilo Bwana Spika mwenyewe. Kuanzia wakati huo mpaka hivi hakujakuwa na mjadala kwamba kuhusu Seneta atakayekuwa wa kwanza, pili, tatu au wa nne. Hili ni jukumu la ofisi ya Spika. Sioni kama kutakuwa na tashwishi katika hao Maseneta ambao wamechaguliwa. Kwa maoni yangu, wote watajukumika na wako na taaluma ya kuweza kutekeleza wajibu wao. Asante."
}