GET /api/v0.1/hansard/entries/1199502/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1199502,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1199502/?format=api",
    "text_counter": 292,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante Bw. Naibu Spika. Kwa sababu ya kazi ambazo ziko mbele yetu, nitajaribu kufupisha mazungumzo yangu kidogo. Jambo la kwanza, ningependa kusisitiza ya kwamba katika hizi kamati zote 14 ambazo zimeteuliwa za kudumu, zote ni muhimu. Hakuna hata kamati moja ambayo tunaweza fikiria ya kwamba haitafanya kazi yake ama sio muhimu. Tuna imani kwamba katika wale Maseneta ambao wamechaguliwa katika hizi kamati tofauti, watatuonyesha utendakazi wao na ukakamavu wao. Ninaamini ya kwamba wataweza kuifanya hii kazi. Kuna hizi kamati 14 za Bunge hili letu la Seneti na kila Seneta hapa amewekwa katika ile kamati ambayo pengine alikuwa ameitaka ama ana ujuzi wa hiyo kazi. Jambo la pili ni kwamba Maseneta ni watu ambao wamesoma. Kwa mfano, ndugu yangu Seneta Lelegwe aliingia hapa kama sio daktari, lakini baada ya mihula hii miwili tumekuwa naye, sasa tunaweza kumuita Sen. Dkt. Lelegwe. Kwa hivyo, pongezi sana ndugu yangu. Pia tuko na wengi ambao ni wafanyibiashara kama dada yangu Sen. Keroche. Yeye pia ni Seneta aliye na ujuzi wa hali ya juu, ambaye atachangia kulingana na ule utendakazi wa hili Bunge letu la Seneti. Kwa hivyo, niko na imani ya kwamba katika ile Kamati ambayo Seneta yeyote amewekwa, anaweza kuifanya ile kazi na ikaonekana wazi. Jukumu ni kwamba sisi sote hapa, tunapiganina serikali za mashinani. Hilo ni jambo ambalo lazima tulizingatie sana. Ya kwamba, katika kazi zetu za utendakazi wote ambao tutakuwa tukifanya, Kamati zetu nyingi zitakuwa zinahusika na mambo ya ugatuzi. Ninaweka mkazo zaidi ya kwamba, katika hizi Kamati zote tulizonazo, kila Seneta ana jukumu na matunda tutayaona hapa yakizaliwa. Nina imani tutazidi kuangalia mbele tukijua ya kwamba kazi itafanywa na Maseneta waliochaguliwa hapa. Kwa hayo machache, Bw. Naibu Spika, naunga mkono."
}