GET /api/v0.1/hansard/entries/1199565/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1199565,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1199565/?format=api",
"text_counter": 355,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika kwa hii fursa ili kuchangia kwenye hii Hoja kuhusu orodha za kamati. Kazi nyingi ya Bunge hufanywa katika kamati. Huwa tunaleta ripoti kutokana na kamati. Kazi ya Mbunge ni kutunga sheria, uangalizi na uakilishi. Katika miaka yangu mitano ambayo nimefanya kwenye Bunge la Seneti, tumefanya kazi nyingi kwenye hizi kamati. Nashukuru kamati za hapo awali. Tumeenda Taita Taveta Kaunti na kamati tano na kufanya kazi nzuri kwa wale wananchi. Ningependa kujihusisha na matamshi ya Seneta wa Nyamira wakili Omogeni aliposema kwamba uongozi wetu ambao umewekwa, uko na tashwishi. Alisema uongozi wa walio wengi ni mzuri. Nashukuru Kiongozi wa Seneti wa Walio Wengi, Mhe. Seneta wa Kericho, kijana mdogo, na mtanashati, vile anavyoongoza ule upande. Ni vizuri tuangalie vile uongozi wa walio wengi wanavyohudumia watu wao. Vile nimeona kwetu, viongozi wetu wamejipatia makuu na kujipa kamati nyingi. Kama kuna jina la kutumia, ni ulafi. Ukichaguliwa usijipatie wewe, patia wengine kwanza. Hii ni nyumba ya kumbukumbu, na kama hivi ndivyo viongozi wetu watatuongoza kwa miaka mitano, basi Kenya Kwanza iwe tayari kuongoza kwa miaka 10 inayokuja. Huu ni uongozi wa ulafi, haueleweki na ni wa kujitakia makuu."
}