GET /api/v0.1/hansard/entries/1199645/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1199645,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1199645/?format=api",
    "text_counter": 435,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Ningependa kuomba Serikali kuu - tunasema asante kwa sababu tayari wameendelea kujizatiti - waweze kupatia watu chakula. Lakini, waongeze bidii. Wapeleke chakula hasa kwa mashule zetu kwa sababu ukitembea katika shule nyingi unapata watoto hawasomi na hawaendi shule. Kwa hivyo, tunaomba ya kwamba ile chakula ambayo imepatikana, kama ni mahindi, mchele ama maharagwe, yote kwanza ipelekwe shuleni ili watoto waweze kusoma na kuhifadhiwa katika shule zao. Bw. Spika wa Muda, jambo la pili ni kwamba, janga la njaa limekuwa ni donda sugu. Mwaka nenda, mwaka rudi, tunaongea kuhusu janga la njaa. Kwa wakati huu, Serikali kuu inafaa ichukue jukumu lake la kusaidia, haswa mambo ya mbegu kufanya utafiti, tuwe na mbegu ambazo zitaweza kuhimidi wakati wa ukame. Tuweze kutafuta njia mbadala, badala ya kutegemea mvua kila wakati. Tuweze kujenga mabwawa ya maji, tutengeneza sehemu zetu ambazo zitakuwa na maji. Hii ni kwa sababu ukiangalia sehemu nyingi, unapata kukinyesha maji yote yanateremka yanaenda katika maziwa na unapata tunabaki katika hali ya ukame. Kwa hivyo, ningependa kuhimiza Serikali kuu iongeze pesa kwa shughuli hii. Hasa sisi watu wa Laikipia, ukitembea mahali kama Dodo, Kimanju, Olmoran, Timau na Matanya, watu wanaishi hali ya uchochole kwa sababu ya hili janga la njaa. Kwa hivyo, naomba gatuzi zetu, hasa Gavana wetu wa Kaunti ya Laikipia, wawache kufanya maendeleo mengine yeyote sasa tuzingatie mambo ya kupigana na bala hili la njaa. Mambo ya kilimo tayari yamepelekwa katika ugatuzi. Kwa hivyo, gatuzi zetu washughulikie mambo ya kupigana na hili baa la njaa. Hata wao, washughulikie mambo haya kwa uadilifu kabisa. Na wale ambao wanafanya utafiti; kwa sababu najua hizi taasisi ambazo ni za utafiti ziko katika Serikali kuu zikuwe zikiangazia mambo ya kutafuta njia mbadala, badala ya kila wakati tunasema mvua ukinyesha, basi mambo iko sawa sawa. Ni jambo la kuvunja moyo ukitembea mahali kama Trans Nzoia, mahali Sen. Mandago ametoka na Bungoma unapata kuna Mahindi. Tungeomba Serikali inunue mahindi kutoka kwa wale watu wa Trans Nzoia, Uasin Gishu na Bungoma waweze kuleta katika sehemu ambazo kuna ukame; mahali kama Laikipia; Maina Village, Rumuruti, na Thome kwa sababu hizo ndizo sehemu ambazo watu wana njaa zaidi. Ningependa kumuomba Rais wa Jamhuri ya Kenya aweze kusema ya kwamba, kumekuwa na janga la ukame ili tuweze kulishughulikia hili jambo kwa hali ambayo inayo faa. Tayari tumesema kwamba kilimo kimeletwa katika gatuzi zetu. Wanaweza kusema wamenunua mahindi na chakula ili watumie hiyo kama sababu ya kutumia pesa zetu vibaya. Kwa hivyo, ningependa kuwaambia Sen. Ali Roba, Sen. Chute na Maseneta wote walio hapa kama vile Maseneta wa kutoka Garissa, Taita-Taveta na Nyeri tukae ngangari. Hiki kinaweza kuwa ni kisingizio cha magavana kupata njia ya kujitajirisha na pesa zetu. Kwa hivyo, tunawaambia, tuko macho, tuko chonjo, tuko ngangari na tutaangalia."
}