GET /api/v0.1/hansard/entries/1199973/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1199973,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1199973/?format=api",
    "text_counter": 274,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "kuishauri Serikali. Sijui ni kwa nini tunachukua madeni mengi sana nje lakini mambo yale muhimu katika taifa hili hatuyaangalii kwa kina. Imekuwa miaka mingi tangu watu wa Kaskazini Mashariki walie juu ya ukame, watoto wao na mifugo kufa, mifugo wanahangaika ilhali hapa Bungeni tunakunywa chai, tunakula chakula cha mchana na jioni tunapotoka tunapata chai. Imekuwaje Wakenya wanahangaika sana kule Kaskazini Mashariki na katika sehemu zingine kame? Ningependa kuishauri Serikali kwamba inasikitisha sana kuwa tumeweza kukopa pesa kwa wingi mpaka imefika trilioni kadhaa. Hizi pesa tunapozikopa inafaa tuziweke kwenye mabomba ya maji kutoka sehemu ambako kuna maji na tuyapeleke hadi sehemu za Kaskazini Mashariki ili tuweze kufanya unyunyizaji ili wakazi waweze kukuza mimea, wanyama wapate chakula na watu wa Kaskazini Mashariki waseme “kwaheri” kwa hali halisi ya njaa na ukame.” Ningependa kusisitiza sana maana hili si jambo ndogo bali ni kubwa sana na linatuhusu sote. Kama Wabunge, tunafaa kushikana kwa huu Mswada maana wenzetu wako na msiba mkubwa sana ilhali wao pia ni Wakenya. Tunafaa kushauriana na pia tuangalie kile tuko nacho mfukoni mwetu ili tuwasaidie hasa wakati kama ambapo Serikali inadai haina pesa, jambo ambalo linatatiza zaidi. Janga la njaa ni dharura kubwa, kama unavyoashiria Mjadala huu wa leo. Ninaomba Serikali ya Kenya itilie maanani na kulishughulikia jambo hili kwa kina. Pia, ningependa kuwaeleza watu wangu wa Mwakirunge, ambao wamo humo humo, kuwa; ijapokua haionekani zaidi, pia nao wanahangaishwa na njaa. Baa la njaa limeshika sehemu kubwa katika taifa hili. Watu wengi ni maskini, hawana makazi na hawajui watashika mti gani. Kwa hivyo, ningependa kuwashauri tuangalie zile sehemu zilizoathirika na njaa ili tuweze kuweka msukumo utakaomaliza hili janga kabisa. Tusiwe tu watu wa kujadili swala hili kila siku ndani ya Bunge. Serikali inafaa iwajibike, pesa zikija watu waache kuitapeli na tuache kuwa na utapeli katika pesa za Serikali maanake utapeli ndio unaoleta matatizo zaidi. Pesa hizi zitumike katika sehemu mwafaka na hitajika ili tuweze kufikia malengo ya kuweza kuwa na taifa huru bila njaa. Jambo lingine ambalo ningezungumzia katika sehemu hizi ni kuhusu mayatima ambao wanahangaika sana. Zamani tulikuwa na mfuko wa mayatima. Sasa hivi na hili janga la njaa, mayatima pia wanahangaika. Kama mama msimamizi wa Mombasa Kaunti, ningependa kusema kuwa mayatima waangaliwe na wapewe mfuko utakaowawezesha kujisaidia. Nitakalolizungumzia la mwisho ni kuhusu wakulima. Inapofika wapewe mbolea, wahusika wasiangalie sehemu moja bali wakulima wote katika taifa zima. Kuna sehemu nyingi ambazo ziko na mashamba. Pengine leo sisi watu wa Mwakirunge tungekua kule Voroni tungekua tumezalisha chakula ili tumsaidie ndugu yetu Wario na watu wetu wa Kaskazini Mashariki. Lakini kwa vile…"
}