GET /api/v0.1/hansard/entries/1199987/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1199987,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1199987/?format=api",
"text_counter": 288,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Mwanzo, ningependa kuchukua nafasi hii kukupongeza kwa kupata nafasi ya kuwa Naibu wa Spika. Tunajua wewe ni mtendakazi. Tunajua kazi yako ni nzuri na tayari ishaanza kuonekana. Kusema kweli, kiangazi kinawatatiza sana watu wetu; haswa, watu wangu wa Lamu Mashariki. Kiangazi kimewaathiri watu wa Kiunga na watu wa Eneo Wodi ya Faza. Ningeomba Wabunge ama viongozi wa taifa letu wasichukulie hili janga la kiangazi kama janga la watu fulani tu maana linaathiri watu kutoka nyanja zote. Mfugaji akipata hasara kwa minajili ya ng’ombe wake kufa, hatakuwa na kitu cha kuuza ili apate faida ili imuwezeshe kupata hela za kununua mazao. Na iwapo mkulima hataweza kununuliwa mazao, itamuathiri pia maana hataweza kufanya ukulima. Hali hii itachangia janga la njaa, ambalo litaathiri afya na elimu. Endapo kiangazi ni kingi, ni lazima rasilimali ya taifa itumike. Huduma za afya zinatakiwa ziwasilishwe kwa wananchi. Ninawaomba viongozi katika Serikali hii wasione hili janga kama ni la watu wachache tu. Mhe. Naibu Spika, katika Eneo Bunge la Lamu Mashariki, ukame unasababishwa na binadamu. Unasababishwa na ndugu zetu majirani. Hivi sasa nikizungumza, watu wa Lamu tulikuwa tumejipanga vizuri. Tuna vidimbwi vya maji ambavyo tumejengea watu wa Kiunga. Lakini katika Eneo Bunge la Lamu Mashariki, ng’ombe hata kutoka Mandera wako huko. Ng’ombe zaidi ya 20,000 kutoka Garissa na Tana River wako malishoni katika maeneo ya mpaka wa Kenya na Somalia. Wametuvamia sisi watu wa Lamu. Maji na nyasi zile zingeliwasaidia wafugaji wetu hata wasingepata shida ya ukame. Lakini saa hii wafugaji kutoka kaunti jirani wamekuja na mifugo wao na kuvamia eneo hilo, na hatuwezi kuwafukuza kwa sababu ni majirani."
}