GET /api/v0.1/hansard/entries/1199988/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1199988,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1199988/?format=api",
    "text_counter": 289,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Nasi pia sasa tumekuwa kwa janga hilo la ukame ilhali tulikuwa tumejipanga. Kwa hivyo, nataka kuwaambia majirani zetu wa Garissa, Tana River na wale wote wanaoleta ng’ombe – hata wanaowabeba kwa malori wakiwaleta – wajue siku ile mimi napigania mabwawa na vitu vingine kupelekwa Lamu wao huwa wako mbele kupigania Lamu isipate mabwawa hayo ili wapate wao. Lakini saa hii tumeona kwamba yale mabwawa machache ya Lamu ndiyo wanayoyafuata. Kwa hivyo, Mhe. Naibu wa Spika, mimi ningeomba Serikali iweze kuangalia yale maeneo ambayo yatakuwa yakiwafaa wengine. Pesa zilitolewa yakajengwa mabwawa lakini mvua haikunyesha kule. Mvua imenyesha mahali kama Lamu, na maji yakapatikana. Sasa iwe ni mtindo, Lamu tuwekewe mabwawa na vidimbwi zaidi ndiyo wakati wa ukame majirani wetu waweze kuja kutumia maji hayo bila kutuathiri sisi."
}