GET /api/v0.1/hansard/entries/1199989/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1199989,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1199989/?format=api",
"text_counter": 290,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Kwa hivyo, nyinyi mnaoniangalia vizuri, tena watu wangu majirani wa Garissa, mhakikishe, maanake nyinyi ndio wa kwanza, tukipata hivyo vidimbwi vinavuta Garissa zaidi kuliko Lamu. Na hivyo ndivyo vitu vinawafaa. Saa hii watu wangu wanatatizika. Changamoto za usalama zinaongezeka kwa sababu ng’ombe na wafugaji ni wengi kwenye misitu, na katika misitu kama Boni kuna matatizo. Kwa hivyo, mnanipatia kazi ngumu mno. Kwa sasa hivi ni wakati mgumu kwa watu wa Lamu, haswa watu wa Kiunga. Kule kwenyewe kuna shida za kiusalama ilhali watu na mifugo wanakuja kwa wingi kudhoofisha usalama zaidi. Kwa hivyo, wakati mwingine mnapopanga jambo lolote kama jambo la msaada kwa upande wa kiangazi, itabidi muihusishe Lamu maana mwafahamu kuwa sisi ndiyo wenyeji wenu. Inafaa Lamu ipate mgao mwingi zaidi ili iweze kuwakaribisha hadi wageni wakati wa kiangazi. Ahsante Mhe. Naibu wa. Spika."
}