GET /api/v0.1/hansard/entries/1200016/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1200016,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1200016/?format=api",
    "text_counter": 317,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Namshukuru Mhe. Rais kwa kurudisha huduma za utendakazi wa bandari kwa Wapwani. Tunawaomba wawekezaji warudi ili watumie fursa hiyo ili vijana wetu wapate ajira. Pia, bandari irudishe ile mfumo wa zamani wa ‘white card’ ili watoto wetu waendelee kupata ajira. Watoto wetu wamekaa mabarazani. Tuna imani kwamba ikiwa watarudisha hiyo ‘whitecard’ itatusaidia zaidi ili watoto wengi waajiriwe. Kutakuwa na moyo na hata wao watakuwa na ufahamu kwamba baada ya muda fulani, watarudi kufanya kazi na wengine watabadilishana baada ya miezi mitatu."
}