GET /api/v0.1/hansard/entries/1200018/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1200018,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1200018/?format=api",
"text_counter": 319,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": "Upande wa Kisauni, amri za kufukuzwa nyingi zimetoka. Hatuingilii mahakama lakini tunaomba wawe na utaratibu wa fikra kwamba unapotoa amri ya kufukuza nyumba zaidi ya elfu moja, unaleta matatizo makubwa. Wanaoteseka ni akina mama na watoto wakati nyumba hizo zinabomolewa. Wale ambao wanadai kuwa zile ardhi ni zao walikuwa wapi wakati ambapo watu walikuwa wanajenga msingi, wakajenga hadi wakaweka paa na stima? Mbona watu hawa wakuje wakati mtu amelala kusema ni kwao? Kwa hivyo, naomba mahakama iwe inaangalia sana swala hilo. Katika upande wa ukame, ningeomba kwamba ukame uwe janga la kitaifa kwa sababu kuna watu wanapata dhiki kubwa wanapoenda hatua ndefu kutafuta maji. Mifugo wanakufa barabarani wanapokosa lishe. Ni vyema taifa liwe na mipango. Wasingoje mpaka wakati kuna ukame wa jua kali ndiyo wazungumze. Kuwe na mpango katika kila kaunti ili kuwe na namna mbadala ya kila jambo. Kama ni water bowsers ama chakula katika maghala, wakati kuna jambo kama hili, kila kaunti ihakikishe inatatua jambo hili. Wasingoje mpaka janga liwe kubwa, tuwe tunakuja kuweka bendera juu ya malori hapa Nairobi ilhali kufika huko pia inagarimu siku kadhaa. Kwa hivyo, mimi naomba mipango hii iwe inashughulikiwa kikamilifu. Kisauni ni sehemu moja kame pia kwa sasa. Ningeomba pia katika yale majina ama ile miji iliyohesabiwa wasitenge Kisauni. Jua limewaka sana kule. Ikiwa chakula kitapeanwa, watu wa Kisauni pia waweze kupata. Kwa haya mengi, nasema ahsante sana. Ikiwa itawezekana, naomba ‘nidoneti’ muda wangu uliobaki kwa Mheshimiwa Mishi hapa. Ahsante sana."
}