GET /api/v0.1/hansard/entries/1200024/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1200024,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1200024/?format=api",
"text_counter": 325,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
"speaker": null,
"content": " Asante Mhe. Naibu Spika. Kwanza, nachukua nafasi hii kukupongeza kwa kuchaguliwa kuwa Naibu wa Spika wa Bunge hili la Kumi na Tatu. Vile vile, kwa haraka, nachukua fursa hii kuwarudishia shukrani watu wa Magarini kwa kuwa iliwapendeza kunichagua kwa mara ya nne kuwawakilisha na kuwafanyia maendeleo. Swala lililo mbele yetu la ukame ni swala sugu ambalo linahitaji kufanyiwa mipango kabambe. Tunapaswa kumudu sehemu kame zote ili ziweze kubadilika na kuwa za manufaa kwa wananchi wetu. Mfano ni eneo la Chakama katika eneo Bunge langu. Ndio, sehemu hii ni kame lakini ardhi ile ina maji ya kutosha. Kinachohitajika tu ni Serikali kuchukua mikakati inayofaa na kuchimba visima ambavyo vinaendeshwa na nguvu za jua na hivyo kunyunyiza maji kwa mashamba na watu waweze kupata chakula cha kutosha. Vile vile, sehemu zingine kama vile Kanagoni ambazo zimepakana na Mbunge aliyeleta Mswada huu ni sehemu kame. Lakini, ndani ya ardhi hizi, kuna maji ya kutosha ambayo yakiwekewa mikakati inayofaa yanaweza kusaidia wananchi kujiendeleza na kupata chakula cha kutosha. Nikimalizia, tunao mradi mkubwa ndani ya kaunti za Tana River na Kilifi ambao hautusaidii kwa njia yoyote ile. Nitamuuliza mwenzagu, Mhe. Ali Wario, tulete Mswada ambao utarudisha mradi huo kwa kaunti hizi mbili ili tuweze kuutumia vyema na watu wetu wasiwe wa kuhangaishwa na njaa kila wakati. Watoto wengi wameacha kusoma kwa sababu ya ukame na njaa. Shule nyingi zinaelekea kufungwa kwa sababu wanafunzi ni haba. Mheshimiwa Naibu Spika, ninaamini ya kuwa Serikali ya Rais William Ruto inaenda kubadilisha maisha ya jamii kwa kuzingatia yale ambayo wameyapanga kwa kuhakikisha ya kwamba wanayafanya yawe ya kweli. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}