GET /api/v0.1/hansard/entries/1200030/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1200030,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1200030/?format=api",
"text_counter": 331,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Kwanza ningependa kukupatia hongera kwa kuweza kuwa Naibu Spika wa hili Bunge la kitaifa. Umeweza kuweka nyota ya kina mama ing’are sana katika taifa letu la Kenya. Pia, ningependa kuwapongeza Spika Mhe. Wetangula na pia Mhe. Kingi ambaye ameweka historia kuwa Spika wa kwanza kutoka Pwani, Kaunti ya Kilifi. Hongera sana. Niwashukuru pia wakaazi wa Likoni na wapiga kura kwa kuweza kuwa na imani na mimi kuweza kunirudisha tena kuwawakilisha ili niweze kuendeleza maendeleo endelevu. Haswa leo ningependa kuzumgumzia Hoja hii ya tharura ambayo inazungumzia janga la njaa na niseme ni ukweli takriban zaidi ya watu milioni tatu hivi sasa wamekosa usalama wa chakula katika taifa letu la Kenya. Ukiangalia katika Mkoa wa Pwani, sehemu za Tana pale, sehemu za Kilifi, Kwale na pia upande wa North Eastern, ambapo ni kule tuseme Kaskazini Mshariki na pia sehemu za Ukambani na sehemu zingine za Kenya, tumeweza kuwa na ukame na kiangazi kikali sana. Hii ni kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa. Swala hili limekuwa swala nyeti na la kilimwengu ambapo inahitajika tuweze kuangalia sera mahususi ambazo zitapambana na hali hii ya hewa ambayo inatuletea ukame wa hali ya juu sana. Tuweze kuangalia nchi ambazo zimeweza kustawi ama kubobea, kwa mfano Misri na Israeli. Hizi ni nchi ambazo zimekuwa na ukame na zimekuwa za jangwa lakini tunaona ya kwamba wanaweza kupata mazao, chakula na wanaweza kuwa na usalama wa chakula katika taifa lao. Ningependa kuzungumzia madhara yanayotuvika tukiwa na janga la ukame. Tunakuwa na ndoa za haraka kwa sababu mabinti wetu wanatembea kilomita nyingi wakitafuta chakula. Hivyo wanaweza kupambana na wale mababa wa sukari na kuweza kupata ndoa za haraka. Hili ni jambo ambalo pia linaadhiri elimu katika taifa letu la Kenya. Wanafunzi pia wanashindwa kwenda shule kwa sababu ya njaa, hivyo pia elimu inaweza kudorora. Vile vile, tunaona misafara ya mifugo ikitoka sehemu kadhaa kwenda kutafuta mahali ambapo wanaweza kupata nyasi ama chakula. Jambo hili linaleta uhasama katika jamii zetu na kuleta shida na vita vya kikabila. Kwa mfano, kuna ngamia wengi wanaotoka katika sehemu ya Tana River, sehemu ya Mashariki Kaskazini, wanaotembea mpaka kule Taita Taveta na Kilifi. Hivyo basi, wakaazi wa kule wanaweza kuona ya kwamba huo ni uchokozi na kunaweza kuwa na uhasama wa kijamii. Haya yote yanaletwa na janga la chakula la kitaifa. Mheshimiwa Rais katika Hotuba yake aliweza kuzungumzia kwamba ni lazima tujenge uwezo wa kulima, uvuvi na tuhakikisha uchumi wa samawati ambao tunaita blue economy uboreshwe ili pia tuweze kupata chakula. Leo uchumi wa samawati unaweza kuleta kilimo cha samaki ambacho hakitakuwa lazima tu kwa wale wanabahari ama ziwa. Hata kule ambapo hakuna kunaweza kutengenezwa mabawa na njia za kilimo cha samaki. Hiyo pia ni njia moja ya kuhakikisha kwamba tuna usalama wa chakula. Kule Pwani, maeneo ya Kwale, Kilifi na Mombasa, tunakosa maji na tuna ule mradi wa Mzima Springs II. Mkoloni alianzisha Mzima Springs I lakini haiwezi kutosheleza hivi sasa asilimia ya Wakenya ambayo imeongezeka marudufu. Kwa hivyo, lazima Serikali iliopo iangalie Mzima Springs II ili tuweze kuboresha chakula. Vile vile, tuwe na sera za kupambana na majanga ya kitaifa. Vile vile, vyakula vya misaada viende kwa wale ambao wanahusika, isiende kwa watu ambao hawahusiki. Vile vile, tuwe na mpangilio ya chakula kwa watoto wetu wa shule ili tuweze kuboresha elimu haswa kwa wakati huu wa janga hili ambalo tuko nalo. Vyakula vyetu vya utamaduni kama ugali, mchele na vyakula vya nafaka viwekwe kwa bei ya chini kwa sababu Mhe. Rais alisema ataaangalia mahasla."
}