GET /api/v0.1/hansard/entries/1200045/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1200045,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1200045/?format=api",
    "text_counter": 346,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
    "speaker": null,
    "content": "Aliye mbele yenu ni Mheshimiwa Fatuma Masito, kiongozi kutoka Kwale. Pili, nashukuru Mheshimiwa Naibu Spika kwa kuchaguliwa Naibu Spika wa Bunge hili. Pia, nampa kongole Mheshimiwa Wetangula kwa kupata nafasi hiyo ya Spika. Tatu, nashukuru wananchi wa Kaunti ya Kwale kwa kunipatia nafasi hii, kwa kunichagua tarehe tisa mwezi wa nane na kusema, “Fatuma Masito, nenda katika Bunge la Taifa ukatuwakilishe”. Wenyewe wananiita Samia Suluhu. Fatuma Masito amezaliwa katika Kaunti ya Kwale. Nimesoma katika Kaunti ya Kwale. Nimeolewa katika Kaunti ya Kwale. Nafanya kazi hii ambayo nimetumwa katika Bunge hili la Taifa ndani ya Kaunti ya Kwale. Nikisema hivyo nina maana ya kuwa ninaielewa Kaunti ya Kwale vizuri sana. Hoja iliyo mbele yetu imeletwa na ndugu yetu, Mheshimiwa Ali Wario, na inasema kuwa janga la njaa au ukame litangazwe kuwa janga la kitaifa. Kaunti ya Kwale ni moja ya kaunti ambazo zimekumbwa na janga hili la ukame. Tukiangalia sehemu za kaunti ndogo za Kinango na Lunga Lunga, na baadhi ya sehemu za kaunti ndogo ya Matuga, zinaumia sana. Sehemu hizi zimepigwa pakubwa na janga hili la ukame. Kuna sehemu iitwayo Marere ambapo maji yanakauka. Maji haya ya Marere yanatoka Kwale lakini yanatumika katika kaunti nyingine. Wananchi wa Kwale wanakufa kiu kwa sababu inasemekana kuna sheria ya miaka ya sitini ambayo inasema maji haya yatatumika katika sehemu nyingine za taifa hili kwa kuwa maji ni haki ya Mkenya yeyote yule. Lakini Mkwale anaumia. Napata kuwa kuna vidimbwi vikubwa vikubwa sehemu nyingine za Kenya, lakini bado Kaunti ya Kwale haijabahatika kupata vidimbwi hivyo vikubwa kusaidia kaunti ile."
}