GET /api/v0.1/hansard/entries/1200046/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1200046,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1200046/?format=api",
    "text_counter": 347,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
    "speaker": null,
    "content": "Sehemu kubwa ya Kaunti ya Kwale ni ya ukulima. Hata hivyo, ukulima hauwezi kufanyika kwa sababu hakuna maji. Katika ile hotuba ya Rais, naomba Kwale iwe kati ya kaunti zitakazotambuliwa na kusaidika. Ndio maana niko hapa ili niwakilishe wananchi wa Kwale walio na kilio kikubwa. Hivi sasa, ninapozungumza, kuna wanyama wameletwa sehemu ya Kwale. Maelfu ya ngamia na ng’ombe ambao wametoka sehemu tofauti tofauti wako Lunga Lunga na Kinango. Kwa sababu sisi Wakwale ni wakarimu, tumenyamaza lakini tunaumia. Imezidi kutuumiza kwa sababu ya janga hili. Imezidi kufagia nyasi, mifugo na hata mchanga wetu. Endapo mvua itanyesha wakati wowote kutoka sasa, basi Kaunti ya Kwale itakuwa katika zile kaunti zitakazoathirika na mmomonyoko wa ardhi. Nikiangalia, kaunti nyingine ziliboreshewa mimea yao katika Serikali iliyopita. Mfano wa hii mimea ni pamba, kahawa na majani. Kaunti ya Kwale ina mimea takribani kama mitatu: Korosho, mnazi na mzingefuri, lakini haijawahi kuboreshwa. Haijapatiwa pesa ya kuboresha mimea hiyo hata siku moja. Ndio maana Mhe. Naibu Spika, watu wa Kwale walinichagua wakasema niende katika Bunge la Kitaifa nikawalilie kilio chao. Ninaomba Serikali hii isaidie watu wa Kwale. Ninaunga mkono Hoja hii ambayo inasema janga la ukame litangazwe kama janga la kitaifa."
}