GET /api/v0.1/hansard/entries/1200365/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1200365,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1200365/?format=api",
    "text_counter": 117,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "wazee kwa sababu naona vijana chipukizi wameingia hapa kama Masenata kutoka kaunti mbali mbali katika nchi yetu ya Kenya. Bw. Naibu wa Spika, cha muhimu nikuona ya kwamba ile ratiba ambayo imewekwa katika Kalenda yetu imetimia na imekabiliwa kisawa sawa na watu wameweza kufanya kazi zao wanaoziweza. Katika hili Bunge, kuna cheche nyingi ambazo hutokea. Lakini tunavyojua ni kwamba katika Bunge hili, Maseneta hujadiliana kwa njia ya heshima na pia vile vile sio kama kutupiana maji ama kuambiana maneno machafu machafu. Sisi ni watu tumestaarabika hapa na nina matumaini ijapokua tuko na vijana, wataweza kuona ya kwamba kwa upande wa wazee, Bunge la Seneti linaweza kufaya kazi zake namna gani. Bw. Naibu Spika pia kama vile alivyosema ndugu yangu Sen. Cheruiyot, pengine ningeweza kujaza kidogo ya kwamba kuna nafasi nyingi za wale ambao wamekuja hivi sasa kwa mara ya kwanza ndani ya Seneti. Kwa hili Bunge huwa na mambo mengi. Sio mchezo wa kandanda pekee yake, kuna pia wakimbiaji. Kwa dada zetu, kuna mpira wa vikapu au netiboli na pia kuna mchezo wa kupimana misuli. Bw. Naibu Spika, ukiangalia pande zote mbili, utaona kwamba Upande wa Walio Wachache, hakuna wanachama wenye misuli. Lakini, Upande Wa Walio Wengi, kuna wale walio na misuli na watacheza mchezo wa kuvuta Kamba. Kwa hivyo, michezo ni nyingi. Afya ya Maseneta ni muhimu. Kwa hivyo, kila asubuhi ama jioni na wakati wowote ule, kuna mahali ambapo mnaweza kwenda kufanya mazoezi ili kuweka akili na miili yetu katika hali ya afya. Vile vile, safari zipo. Safari zitakuwa nyingi. Ninakumbuka mimi nimeenda safari na ndugu yangu Sen. Kinyua. Vile alivyosema Ndugu yangu, Sen. Cheruiyot, yeye yuko sawasawa. Yeye ni mtu wa shughuli nyingi, lakini yale anayo ya shughulikia, anayaelelewa vizuri. Mimi nilimsindikiza tu pande zingine. Katika kunyoosha misuli, vile, siwezi kujua tumejitayarisha kivipi kwa michezo. Maanake, kwa hii michezo ambayo itakuwa East Africa Legislative Assembly (EALA) kama vile nilivyotangulia kusema, itakuwa michezo kadhaa wa kadhaa. Hivyo basi, tutatakikana tuwe na akina dada zetu. Nikiwaangalia hawa dada zetu walioko hapo, nahofia kuwa wanaweza kufungwa mabao mengi sana. Sioni yule anayeonekana mkakamavu. Labda Sen. Keroche anaweza kujaribu. Hizi ndizo mbinu mbalimbali ambazo sisi tutaweza kufanya muhula huu. Kuanzia sasa hadi Disemba---"
}