GET /api/v0.1/hansard/entries/1200477/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1200477,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1200477/?format=api",
    "text_counter": 229,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": ". Sisi tunawatakia mema. Ni vizuri wamekuja kuona mambo ambayo tunayoyafanya hapa Seneti. Nawasihi watie bidi kwa masomo yao kwa sababu masomo ndio uti wa mgongo wa maendeleo katika nchi yetu ya Kenya. Ijapokuwa wamekuja hivi leo na wakatupata tukiendelea na shughuli zetu za kujadili, ni bora wajue eti mijadala huendelea vivyo hivyo. Kuna hoja za nidhamu. Mambo mengi hutendeka hapa. Kwa hivyo, wakija wakati mwingine, watatupata tumevulia njuga maswala muhimu ambayo tunapaswa kuangalia. Siku ya leo, tulikuwa tunaangalia mambo ya kalenda yetu. Kwa hivyo, hatujaanza mijadala ya kusisimua, tunayoweza kujadili kwa mapana na marefu. Nawakaribisha na kuwatakia mema katika masomo yao. Ningependa wajue ya kwamba, mawingu ndipo mahali ambapo watakapofika. Najua watakuja hapa Seneti. Seneti ndilo Bunge ambalo linajulikana kwa kujadili Miswada ambayo ni muhimu sana katika Jamhuri yetu ya Kenya. Nawakaribisha sana na kuwatakia mema siku za usoni. Bw. Naibu wa Spika, asante kwa kunipa fursa hii."
}