GET /api/v0.1/hansard/entries/1200480/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1200480,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1200480/?format=api",
    "text_counter": 232,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13592,
        "legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
        "slug": "onyonka-richard-momoima"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, natoa shukrani zangu kwa kunikubalia nizungumze kwa ufupi sana. Ningependa kuwaambia wanafunzi ambao wamekuja hapa kwamba Kenya ni nchi nzuri ikiwa tutailinda. Najua wamekuja hapa kuelewa vile tunavyojadiliana kama viongozi, kwa maswala nyeti yanayohusu wananchi wa kawaida ili tuweze kuboresha maisha yao. Naona wengi wao ni wasichana na ningependa kuwaambia ya kwamba Kenya ni nchi ambayo inalinda haki za wasichana au wanawake kikatiba. Haki hizo zinawapa nafasi ya kuendelea ili hao pia wawe viongozi wa kesho. Natoa shukrani zangu kwa waalimu wao ambao wamewaleta hapa. Ikiwezekana, wapitie ule upande mwingine wa Bunge la Kitaifa ili pia waone vile wanavyoendelea kujadili na kuzungumzia maswala tofauti. Bw. Naibu wa Spika, asante kwa kunipa fursa hii, kuzungumzia haya mambo."
}