GET /api/v0.1/hansard/entries/1200487/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1200487,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1200487/?format=api",
    "text_counter": 239,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya Kalenda ya Seneti. Kalenda hii itatusaidia kupanga kazi zetu Bungeni na mashinani. Bali na kuhudhuria vikao vya Bunge, kuna ofisi za mashinani ambazo ni muhimu katika kuendesha kazi zetu ili kuhakikisha kuwa kila kitu kiko sawa. Mapumziko haya yatatoa fursa kwa Maseneta kuendelea kusoma. Hapa Bungeni hakuna mwisho wa kusoma. Utakuwa unasoma mpaka siku Bunge litakapojunjwa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2027. Bw. Naibu Spika, nimegundua kuwa mara nyingi Maseneta wa upande wa walio wengi wachache wanatatizika na vifaa vya kisasa viliyoko katika Bunge hili. Mapumziko hayo yatatoa fursa kwao kufundishwa ili wawe sawa katika mambo ya mitandao na waweze kutoa michango yao kiutalamu kama inavyokusudiwa. Nilifurahi Seneta wa Tana River aliposema kwamba Bunge hili linafaa kuwa huru ili kufanya kazi yake kwa kuzingatia masilahi ya Wakenya wote. Naomba upande wa walio wengi wachache wakubali wanachama wa Kamati ambayo tumependekeza wawe na nafasi ya kuteua wenyeviti---"
}