GET /api/v0.1/hansard/entries/1200795/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1200795,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1200795/?format=api",
    "text_counter": 198,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Naitwa Mhe. Zamzam Chimba Mohammed. Ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru wakaazi wa Mombasa ambao walinipa kura zao kwa heshima na taadhima. Nawapongeza sana. Pia, nampongeza pia Kinara wangu wa Chama, kiongozi wangu, Mhe. Raila Amolo Odinga, kwa kuamini wanawake na kutupa nafasi mwafaka. Mwisho, pia tulikuwa hatujui tushike wapi lakini, alitusaidia tukafunga kazi na kupata ushindi. Ningependa pia kushukuru familia yangu yote ambayo ilinishika na kuniombea dua. Nawaambia wakaazi wa Mombasa kuwa nitawafanyia kazi. Nitahakikisha kuwa mtoto wa kike atapewa heshima katika jamii, na atapata nafasi ya pili ya kupata elimu na kuondoa tamaduni ambazo ni potofu. Katika Hotuba ya Rais, ningependa kwanza kumpongeza sana kwa kuturejeshea bandari yetu ya Mombasa. Lakini pia, nina wasiwasi kwa kuwa tetesi zimetoka nyingi kuwa hati miliki ya ile bandari si yetu. Ningependa kumwambia Mtukufu Rais kuwa, kwa hisani yake, heshima na taadhima, afuatilie jambo hili ili wakaazi wa Mombasa wasiwe wakutolewa kafara na bandari yetu ichukuliwe. Wakenya wote wachangie jambo hili. Tuchange pesa hizi tunazodaiwa na Mchina ili zilipwe na Wakenya wote. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}