GET /api/v0.1/hansard/entries/1200796/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1200796,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1200796/?format=api",
    "text_counter": 199,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Ningependa pia kumwambia Rais kuwa tuna maliasili na rasilimali zetu, kama wakaazi wa Pwani, kama vile korosho na madini. Ningependa kumshawishi na kumuelezea kuwa aturahisishie barabara ya Dongo Kundu iweze kufunguliwa mapema, ili tuweze kupata ajira na kufungua viwanda ambavyo vitaleta ajira kwa vijana wetu wa Mombasa. Wengi wamepotea katika mihadarati. Wengine wanachukuliwa na ushawishi mkubwa kwenye mambo ya Al-Shabaab, kwa sababu ya ukosefu wa ajira. Kwa hivyo, namuomba Rais pia atufungulie viwanda. Kenya Meat Commission (KMC) ilikufa Mombasa, lakini inafanya kazi sehemu zingine. Haijafufuliwa Mombasa. Tuangalie viwanda vya korosho, miwa na Kenya Bixa. Vyote vifunguliwe ili wakaazi wa Mombasa na Pwani nzima waweze kupata ajira na kuuza rasilimali zao. Nataka kuzungumzia mambo ya afya. Sote tunaelewa kuwa National Hospital Insurance Fund (NHIF) ililetwa ili kuboresha na kufanya wepesi wa watu kupata huduma za afya. Lakini, wengi wakienda kwenye hospitali, wanaambiwa kuwa NHIF inagharamia pesa ya kitanda na hakuna dawa na huduma zingine ambazo wanafanyiwa. Wazee wengi wamelalamika sana. Kwa hivyo, Serikali iangalie hali katika NHIF, ili tuweze kupata huduma ambayo inatibu maradhi mengi mazito. Kisha nikiangalia mgao wetu wa National Government Affirmative Action Fund (NGAAF) kama akina mama wa kaunti 47, mgao wetu uko chini sana ukilinganisha na kuwa tunafanya siasa kaunti nzima. Ndio maana wengi hawarudi Bungeni. Kwa hivyo, namuomba Rais aangalie hilo kila atakapoangalia NG-CDF na yale mengine ya kaunti. Pia, sisi wanawake katika NGAAF, namuomba aangalie hali zetu ili tupate mgao ambao utatusaidia."
}