GET /api/v0.1/hansard/entries/1200815/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1200815,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1200815/?format=api",
    "text_counter": 218,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kenga Mupe",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "(Rabai, PAA) Ahsante sana Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii nitoe maoni yangu. Kwanza nashukuru Mwenyezi Mungu kwa umbali ambao amenifikisha. Leo niko hapa katika Bunge letu tukufu. Naomba nichukue fursa hii ya kipekee kuwashukuru wakaazi wote wa Eneo Bunge la Rabai kwa kusimama nami. Siku ya kupiga kura walijitokeza kwa wingi kunichagua niwe mtumishi wao. Nataka kuchukua fursa hii kupongeza timu yote ya Kenga Mupe a.k.a Apewe, kutoka Mwawesa Ward, Ruruma, Kambe/Ribe na Rabai Kisurutini. Kwa hakika, walifanya kazi ya maana tena nzuri. Mimi kama mtumishi wao, Mhe. Anthony Kenga Mupe, nawahakikishia wakaazi wote wa Rabai kuwa nitawatumikia pasipo ubaguzi na pasipo kuangalia yule aliyenipigia kura na yule ambaye hakunipigia kura. Mhe. Spika, kuhusu Hotuba ya Rais, ilikuwa safi sana, fupi, nzuri, na ya kuaminika. Kwa sababu katika Hotuba hiyo, alizungumzia suala la maji. Kama tunavyojua, Katiba Ya Kenya katika Ibara 43(1)(d), inamhakikishia kila mtu haki ya kupata maji safi, salama na ya kutosha. Kwa hivyo, nampongeza sana Mhe. Rais kwa hotuba yake iliyoangazia suala la maji. Nikiwa Mbunge wa Rabai, najua tatizo kubwa sana ni ukosefu wa maji. Kwa hivyo, kupitia Hotuba ya Mhe. Rais, sekta ya umma na ya kibinafsi zitasambaza maji kwa Wakenya wote. Napongeza sana Hotuba ya Mhe. Rais. Pia katika Hotuba ya Mhe. Rais, alizungumzia hustlers’ fund. Kupitia hustlers’ fund, vijana wetu watapata nafasi ya kufanya biashara ndogo ndogo. Mama mboga, mama fagio na mama kuuza nazi kutoka Rabai atapata nafasi nzuri ya kujiinua katika maisha. Kwa hivyo, napongeza kikamilifu Hotuba ya Mhe. Rais na ninaiunga mkono kwa sababu imezungumzia zile shida za mtu wa chini hususan kutoka Rabai Sub County. Nikimalizia, nakushuru Mhe. Spika. Wewe ni kiongozi wa chama cha FORD-K na alama yako ni Simba. Ingawa hivyo, juzi wakati ulipokuwa unatoa mwongozo na uamuzi humu Bungeni kuhusu ni nani wengi katika Bunge hili, kwa hakika ulisimama imara kama simba na kuamua kwamba Kenya Kwanza ndiyo ina Wabunge wengi katika Bunge hili. Ahsante sana Mheshimiwa Spika. Nakupongeza wewe na Naibu wako. Mungu aibariki Kenya."
}