GET /api/v0.1/hansard/entries/1201225/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1201225,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201225/?format=api",
"text_counter": 305,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 380,
"legal_name": "Shakila Abdalla",
"slug": "shakila-abdalla"
},
"content": "Bw. Naibu wa Spika, asante kwa kunipa hii fursa kuweza kuchangia Hotuba ya Rais. Kwanza, ningependa kuchukua nafasi hii kuishukuru chama changu kwa kunipatia hii nafasi ya Seneta Maalumu na wale ambao wamechaguliwa kutoka kwa chama changu ambao wameniwezesha kupata hii nafasi. Vilivile, nawashukuru na kuwapongeza nyote ambao mumechaguliwa katika Seneti hii ya ki fahari kutekeleza majukumu yenu. Bw. Naibu wa Spika, Hotuba ya Rais, kwa maoni yangu, haiambatani kamwe na matarajio ya mwananachi. Neno ‘ Hustler’ ambalo huwa linatumika sana kama maua ya kurembesha ama kwa ufasaha na utaalam mwingi haswa na viongozi wa juu, ni neno ambalo halijaweza kupata maana kikamilifu. Kwa maoni yangu, ninaona kama Rais hajiamini ama hana uzoefu wa kuelewa kikamilifu miundo mbinu ya kugeuza uchumi wa nchi na kuinua maisha ya mwananchi. Kuna fiche fiche ambazo zinabainisha kuwa serikali kuu ina upungufu wa kuelewa ajenda zake, mwelekeo wa nchi na uchumi wake. Bw. Naibu wa Spika wa Muda, kuna changamoto ambazo zinatukumba kama za ufisadi, ajira, gharama za juu za biashara, usalama, barabara, miundo msingi, maji safi, uchafuzi wa mazingira na ukusaji wa viwanda. Nataka nitoe mfano wa mbolea. Hivi sasa, bei ya mbolea imerudishwa chini kwa shillingi elfu tatu. Kenya haitaki mbolea za kupewa kama marupurupu na nchi za ng’ambo kwa bei rahisi ilhali hatuzielewi. Kenya inahitaji viwanda ambavyo vitatengeneza mbolea kwa bei nafuu, kukuza mazao yao na kujenga uchumi wa nchi. Hiyo ndiyo itakuwa njia bora ya kuleta mabadiliko na kuendeleza nchi. Kwa njia ya Fuliza, nampongeza Rais kwa kile alichofanya katika Fuliza na M- Shwari lakini tunataka afuate mkondo huo afanye vivo hivyo kwa World Bank na"
}