GET /api/v0.1/hansard/entries/1201227/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1201227,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201227/?format=api",
    "text_counter": 307,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 380,
        "legal_name": "Shakila Abdalla",
        "slug": "shakila-abdalla"
    },
    "content": "(IMF). Hizo ndizo sehemu ambazo zitaleta mabadiliko makubwa ya uchumi wa nchi. Kuna swala la Kshs300 billioni kutolewa. Hivi sasa, tuko na Mawaziri Wasaidizi na hizo ofisi zao haziambatani na Katiba. Hiyo ndio mbinu mwafaka ya kupunguza gharama za Serikali na kuinua uchumi wetu. Rais atoe nafasi za Mawaziri Wasaidizi ambazo ziko pale kuzawadia wale waliomkampeinia. Kuna jambo la kulipa ushuru. Mwananchi mdogo ndiyo unaona anaumizwa sana. Tunataka Serikali ilenge na ipeleke macho yake kwa wale samaki wakubwa. Hao ndio wanafaa kulipa ushuru wa kubadilisha uchumi wa nchi. Tunafaa kuanza na Rais mwenyewe. Katika aya ya ishirini na moja, Rais alisema ya kwamba tunafaa kuinua uchumi kwa kupitia uvuvi. Hivi sasa, kitengo cha uvuvi kimewekwa kwenye idara ya BlueEconomy na uvuvi hapa nchi unafanywa na vijahazi na vidimbwi vya maji. Huu ni uvuvi mgani ambao utaweza kuinua nchi yetu? Utapata ya kwamba wale ambao wanafanya uvuvi kwa vijahazi wanakatazwa kuvua kwa mikano. Hiyo sheria ya mikano inafaa iwekewe matrola wala sio wavuvi wa chini. Sasa wamekatazwa kuvua samaki. Wangefikira kabla ya kutunga sheria hiyo ili wavuvi wadogo wasiathirike."
}