GET /api/v0.1/hansard/entries/1201229/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1201229,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201229/?format=api",
    "text_counter": 309,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 380,
        "legal_name": "Shakila Abdalla",
        "slug": "shakila-abdalla"
    },
    "content": "Kuna upungufu wa samaki nchini. Kenya inahitaji samaki tani milioni 900 lakini tunapata tani milioni 700 pekee. Raslimali zetu zinachukuliwa na watu kutoka nje ya nchi kwa sababu wana mitambo ya kisasa ya kuvua samaki. Kama nchi, tunahitaji kuwa na mitambo ya kisasa ya kuvuua samaki na kufundisha watu wetu mbinu mbadala za kuvua. Endapo tutafanya hivyo, tutainua uchumi wetu na kubadilisha maisha ya mwananchi aitwaye ‘ hustler’. Kwa sasa, raslimali zetu zinachukuliwa na watu ambao si Wakenya. Ukame na mafuriko ni majanga yanayotukumba kila mwaka. Tunashangazwa wakati Serikali inafanya firefighting badala ya kutafuta suluhisho la ukame na mafuriko. Wakati wa mafuriko, maji yanafaa kudhibitiwa. Maji hayo yanaweza kusaidia katika ukulima na kupanda mimea ya kulisha mifugo wetu wakati wa ukame. Tunafaa kujipanga kikamilifu lakini hatuna mikakati. Kila mara, watu hupigana wakati majanga yanapotukabili ilhali hakuna mikakati inayowekwa kukabiliana na majanga yanatukumba kila mwaka. Serikali imeanza kupigana na ufisadi kwa kuwa baadhi ya watu wametiwa mbaroni. Hata hivyo, kusiwe na ubagusi wa vita dhidi ya ufisadi kutegemea mirengo . Yeyote anayeshutumiwa kwa kosa la ufisadi anafaa kupelekwa mahakamani. Isionekane kwamba watu fulani ndio wanaoshitakiwa ilhali wengine wanaachiliwa. Ufisadi ni janga kubwa sana hapa Kenya. Hata uchumi wetu ukiimarika, hatutasonga mbele endapo ufisadi utazidi kukita mizizi serikalini."
}