GET /api/v0.1/hansard/entries/1201316/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1201316,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201316/?format=api",
    "text_counter": 396,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Bw. Naibu wa Spika, ninadhani mimi ni mrefu kidogo sasa nikisimama wima, sijui kama nitafikia kipaza sauti, lakini nitaendelea tu. Hata hivyo, ninazungumza kwa Kiswahili lakini Hotuba ya Rais iko kwa Kiingereza. Kwa hivyo, hakuna uwezekano wa mimi kusoma wakati ninatoa taarifa yangu. Bw. Naibu wa Spika, ninaomba ulinzi ili nimalize kwa sababu niko karibu kusahau ambayo nikuwa ninataka kusema Rais wetu alisema ili tuweze kupata chakula cha kutosha, lazima tufanye kilimo na kupeana mbolea ya ruzuku kwa wakulima. Ninamshukuru Rais kwa sababu tayari ashaanza kufanya hivyo na hiyo mbolea ishafikia wakulima. Hili ni jambo muhimu katika kuongeza chakula inchini. Katika leseni ambazo wauzaji wanahitaji ili kuuza mazao yao katika nchi za nje, Rais alisema ni vizuri tuondoe utawala wa ziada. ili wakulima wapate hizo leseni, ambazo zitawawezehse kuuza mazao yao nje. Ningependa pia kuongezea kwamba itakuwa bora zaidi tukitumia mitambo ya kisasa katika ukulima wa mchele na mahindi, ili kuongeza mazao. Ninamshukuru Rais wetu kwa sababu sasa hivi katika Kaunti ya Kirinyaga, wakulima wanasajiliwa na wataweza kupata mbolea ya bei nafuu. Hii ina maana kwamba wataongeza kilimo. Jambo la pili ambalo ningependa kuzungumzia ni pesa ambazo maskini wanaoitwa hustlers, wanapewa. Ni wazi kwamba kizingiti kikubwa katika ufanyi"
}