GET /api/v0.1/hansard/entries/1201318/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1201318,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201318/?format=api",
    "text_counter": 398,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "biashara kwa watu wenye uwezo mdogo wa kupata fedha ni mtaji au capital kwa Kiingereza. Rais aliahidi kutoa shillingi billioni 50 ili kuinua wafanyi biashara wadogo. Watu wakiinuliwa hivi, wataweza kufanya mambo mengine ikiwemo kusomesha watoto na mambo mengineyo. Jambo la tatu nitakaloliongelea ni sheria. Kuna sheria gandamizi ambazo zimetengenezwa na Bunge na lazima tuziangalie. Nitaongea kuhusu sheria iliopitishwa mwaka wa elfu mbili na kuma na tatu ya shirika la Agriculture and Food Authority(AFA) . Hii sheria ilizuia wakulima kuuza macadamia na korosho bila kuzitoa maganda kwa nchi za nje. Bw. Naibu Spika, sheria zile hazikufaidi mkulima. Mabwenyenye wachache ndio wananufaika kwa sababu wakulima wengi hawana uwezo wa kuweka ile mitambo ya kutoa maganda kwa korosho, macadamia na zinginezo. Ningeomba Bunge hili liweze kutoa zile sheria ili wakulima wengi katika Kenya hii waweze kuuza mazao yao kwa bei nafuu bila kugandamizwa. Kuna dhamana ya viwango ambavyo vitakua vinatumika kulipa wakulima wa kahawa, majani chai na vitu vinginevyo. Katika manifesto ya Kenya Kwanza, tutawapatia wakulima viwango chini vya pesa vya kulimia ili kuwawezesha kulima bila shida nyingi. Inaitwa kwa lugha ya kimombo guaranteed minimum returns. Wakulima wanaolima mchele, ngano na zinginezo wakijua kutakua na kiwango fulani cha pesa, wataweza kujipanga vilivyo ili waweze kutoa hata zaidi kutosheleza mahitaji ya nchi hii. Bw. Naibu Spika, nitaongea kuhusu stima. Nimetaja miradi kama ile ya Tana River na Perkerra. Kuna ile inatumia mashine kutoa stima ambayo inapiga maji kupeleka mashambani. Kama bei ya stima itaendelea kua ghali, itakua ngumu sana kuweza kutoa maji kwa bei nafuu. Katika aya ya thelathini na mbili, Rais aliongea juu ya stima. Ni vizuri ikiwa watu binafsi watawezeshwa kutoa stima kwa bei nafuu. Kuna gazette notice ambayo ilitolewa juzi na serikali iliyoondoka kuongeza bei ya maji. Wakulima mbeleni walikua wanalima ekari moja na kulipia maji shilingi elfu tano. Katika ile gazette notice iliyotolewa, mkulima atalipa shilingi elfu ishirini. Kulingana na taarifa ya Rais, tutakua na baraza jipya la mawaziri hivi karibuni. Waziri wa maji ataangalia sehemu hii na kuitupilia mbali ili wakulima waweze kupata maji na mbolea kwa bei nafuu ndiposa waweze kulima na kupata mapato zaidi. Ahsante sana, Bw. Naibu Spika."
}