GET /api/v0.1/hansard/entries/1201334/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1201334,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201334/?format=api",
    "text_counter": 414,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa ya kuunga mkono Hoja ya Sen. Cherarkey. Bunge hili lilianza kazi hivi karibuni na tumeona kwamba tumekua na vikao ambavyo vimeweza kwenda kwa muda mrefu. Wiki iliyopita tulipokua na kikao cha kwanza, tulikaa hapa mpaka saa moja na nusu. Mhe. Spika Kingi alikaa kwenye kiti kuanzia saa nane na nusu mpaka saa moja unusu usiku tulipohairisha kikao. Hiyo ilikua ni kazi ya ziada kwa Spika kwa sababu alikua peke yake. Leo tumeona ya kwamba umekaa kwenye kiti kuanzia Saa Nane na Nusu mpaka sasa, Saa Kumi na Mbili Unusu. Hii inamaanisha kwamba nyinyi ni viongozi ambao walijitolea kuendesha Bunge hili bila kujali kuchoka au wakati mumekaa kwa kiti. Kwa hivyo, kuchaguliwa kwa Seneta Wakili Sigei na Seneta Abdul Haji kama Maspika mbadala kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge hili utasaidia pakubwa kuendesha shughuli za Bunge hili mpaka wakati ambapo daBunge hili litakuwa na Maspika wa Muda."
}