GET /api/v0.1/hansard/entries/1201374/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1201374,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201374/?format=api",
"text_counter": 454,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Hotuba ya Rais. Kwanza, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa fursa ya kuchaguliwa na wananchi. Vile vile, namshukuru Rias wangu, Mhe. William Samoei Ruto, pamoja na naibu wake, Mhe. Rigathi Gachagua, kwa kunipa fursa ya kuwania kiti cha useneta kwa Chama cha UDA. Pia, nawashukuru watu wa Laikipia kwa kunipigia kura zilizoniwezesha kuibuka mshindi. Vile vile nawapongeza Maseneta waliochaguliwa na wale ambao waliteuliwa. Heko na tutafanya kazi pamoja. Hotuba ya Rais iliangazia mambo muhimu ambayo ananuia kutenda. Nimekuwa nikiwasikiliza wenzangu wakiongea hapa. Ni kana kwamba amefanya mambo aliyoahidi. Ni mambo ambayo ananuia kufanya. Najua na nina uhakika kuwa kuna mambo mengi atakayofanya. Badala ya kupinga, kama Seneta, unafaa kuangalia manifesto ya Mrengo wa Kenya Kwanza ili uelewe mambo ambayo Serikali itafanya. Tunafaa pia kuwapa muda. Sen. Cherargei amesema kuwa Serikali hii haijamaliza hata siku 30. Ni siku chache sana baada ya Rais William Ruto kuapishwa. Hata hivyo, kuna baadhi ya watu wanaokashifu kutotendeka kwa mambo fulani. Seneta wa Homa Bay, Sen. M. Kajwang’, amesema kuwa bei ya bidhaa imeongezeka lakini ukweli usemwe. Waswahili husema; mgala muue na haki umpe. Walipochukua hatamu za uongozi, hazina yetu haikuwa na chochote. Namshukuru Rais kwa sababu hata baada ya hayo, mbolea imepunguzwa bei kutoka Kshs6,000 hadi Kshs3,500. Hilo ni jambo muhimu. Rais pia alisema kuwa tunafaa kubadilisha Kanuni za Kudumu za Seneti na Bunge la Taifa ili kuwe na uwezekanao wa kuwaalika Mawaziri hapa kujibu maswali moja kwa moja. Hilo ni jambo muhimu ambalo tunapaswa kufanya ili kutuwezesha sisi wawakilishi wa wananchi kuuliza Mawaziri maswali moja kwa moja bila ya kutumia kamati zetu jinsi ambavyo tumekuwa tukifanya. Nikiwa Mwenyekiti wa kamati, tulikuwa tunawaalika Mawaziri lakini hawaji. Ikiwa tutabadilisha Kanuni za Kudumu za Seneti, Waziri yeyote atakayealikwa atakuja hapa na hiyo itatuwezesha kupata majibu ya maswali yetu moja kwa moja. Jambo lingine lililonifurahisha ni kuhusu mahakama zetu."
}