GET /api/v0.1/hansard/entries/1201376/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1201376,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201376/?format=api",
    "text_counter": 456,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Rais tayari ameteua Majaji wale ambao walikuwa wamekaa muda mrefu kabla ya kuteuliwa. Halafu Raisi mwenyewe alisema ataongea na Bunge - ataongea na watu ambao wanahusika - ndiposa hela zile ambazo zinatumiwa pale mahakamani ziweze kuongezeka. Hilo ni jambo nzuri na tena mahakama zikipata hela zitaweza kufanya kazi zao kwa uadilifu bila kukaa wakibabaishwa kwa kuwa hawana hela za kutosha. Jambo lingine ambalo limenifurahisha ni kwamba Rais hata ijapokuwa pengine hakulisema hilo jambo lakini tayari amelitekeleza. Maafisa wetu wa usalama wamepewa kitita cha pesa wao wenyewe hawatakuwa wakitegemea ofisi ya Rais wakitaka chochote. Hilo ni jambo nzuri sana kwa sababu mimi nimetoka Kaunti ya Laikipia, mahali mambo ya usalama yamekuwa ni kizungumkuti. Ukienda kwenye kituo cha polisi kutoa ripoti unaambiwa ya kwamba hawana mafuta lakini hilo ni jambo ambalo litakuwa limekwisha kwa sababu watakuwa wakipata pesa zao moja kwa moja, watakuwa wakijitegemea. Kwa hilo, ninampongeza Rais na ninasema tutamuunga mkono mia kwa mia. Jambo lingine ambalo nimeliona ni nzuri tena, amesema ya kwamba Bunge la Seneti na Bunge la Taifa watapata pesa za kuwasaidia katika kazi yao ya uangalizi. Kwa sababu sisi tumekuwa tukifanya kazi hizi zetu za uangalizi unazunguka ukitumia mshahara wako. Inakuwa vigumu sana lakini sasa tukiwa na fedha hizi tutazitumia na hata unaweza kupata wahandisi ambao watakuwa wakiangalia barabara zetu wakitumia fedha hizi. Hili ni jambo ambalo litakuwa la manufaa na kazi tutaweza kufanya kwa uadilifu na itakuwa ni kazi ambayo tunaitekeleza. Kwa sababu imekuwa ni vigumu sisi kama Maseneta kufanya kazi. Unakumbuka tulipigana hapa ilikuwa ni vita vya nguo kuchanika tukijaribu kusema pesa zile zinazoenda katika kaunti zetu ni mpaka ziongezwe. Tulikuwa tupewe Kshs310 bilioni, tukasukuma mpaka tukapata Kshs370 bilioni. Lakini baada ya kupata fedha hizo, sisi tunazipeleka katika kaunti lakini hatuna fedha ambazo zinapaswa kutumika ili tuweze kuangalia zile pesa ambazo tumepeleka katika kaunti zetu. Kwa hivyo ninaunga mkono hizi pesa za uangalizi, ama kwa lugha ya Kiingereza, oversight . Jambo lingine ambalo ninaunga mkono ni fedha za walala hoi ama Hustlers Fund kwa sababu watu wengi wamekuwa wakikimbizwa na kusumbuliwa kama swara. Nimesikia Seneta mmoja akisema hapa ya kwamba ukitembea hapa Nairobi, uende Kirinyaga Road huko Grogan, ndugu zangu wakifanya biashara wanafukuzwa kama swara. Hii ni kwa sababu kuna wale ambao biashara zao ni za kibwenyenye lakini mtu ambaye biashara yake ni ya reja reja yeye haonekani akiwa wa manufaa. Ninataka kumshukuru Rais kwa sababu alisema ya kwamba hakuna biashara ambayo haipaswi kuheshimiwa, iwe mtu anauza nyanya ama vitu vyake vya reja reja, hiyo ni biashara. Kuhusu hizi hela za Hustlers Fund, Kshs50 bilioni, nimekuwa nikiambiwa kwamba wale wafanya biashara reja reja, watu wa boda boda, watu wa sokoni kila mtu anasubiri hizi hela; na ninaona ya kwamba sisi watu wa Laikipia haswa wale ambao wanafanya biashara ya reja reja, wataweza kupata afueni. Hapo mimi ninaunga mkono na ninasema Rais, aendelea kufanya kazi na sisi tuko nyuma yako."
}