GET /api/v0.1/hansard/entries/1201378/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1201378,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201378/?format=api",
    "text_counter": 458,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Jambo lingine ambalo ningependa kuunga mkono katika hotuba ya Raisi, amesema mambo ya nyumba. Ukitembea Laikipia, unapata watu wanaishi katika nyumba ambazo sio nzuri. Ukienda mahali ambapo panaitwa Maina Estate, Majengo-Nanyuki, Riki, utapata watu huko wanaishi maisha duni. Mimi ninaunga mkono vile Rais amesema ya kwamba tutapata nyumba ambazo mtu anaweza akanunua. Hilo ni jambo la muhimu kwetu na ni jambo ambalo tunaunga mkono. Tumeona kuwa Rais anatufikiria kama vile alivyokuwa akisema ni “kusema na kutenda” na mimi ninajua atafanya. Ninakumbuka Rais alipokuwa Waziri wa Kilimo, aliweza kupunguza bei ya mbolea kama vile alivyofanya sasa, kutoka Kshs6,000 kuwa Kshs5,500. Alipokuwa Waziri wa Elimu ya Juu, alipunguza muda wanafunzi waliokuwa wamemaliza Kidato cha Nne walikuwa wanakaa nyumbani kabla ya kujiunga na vyuo vikuu. Walikuwa wanakaa zaidi ya miaka miwili kabla kujiunga na vyuo vikuu. Alipunguza muda huo hadi miezi sita. Ikiwa wakati huo aliweza kufanya hivyo na hakuwa na mamlaka kama haya aliyonayo akiwa Rais, sembuse sasa? Bw. Spika wa Muda, nina imani ataweza kutenda yote ambayo ametuahidi. Ningependa kuwaambia wale ambao wanapinga kidogo kwamba Mswahili husema, subira huvuta heri. Mngoje na msikate kanzu kabla mtoto kuzaliwa. Nimeona Rais wetu akishugulikia mambo ya walala hoi. Ameongea kuhusu fuliza, M-shwari na kusema ya kwamba ruzuku iliyokuwa ikitozwa itapunguzwa mpaka iwe asilimia 40. Naona ya kwamba Rais yuko chonjo na tayari kutenda kazi. Bw. Spika wa Muda, ningeomba tumuunge mkono. Wale ambao wanaona mambo hayafanyiki, ni siku chache. Yuko na muda wa miaka mitano na baada ya hiyo miaka, ataweza kufanya yote. Nashukuru sana, Bw. Spika wa Muda."
}