GET /api/v0.1/hansard/entries/1201400/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1201400,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201400/?format=api",
"text_counter": 480,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, nakushukuru kwa hii fursa umenipa ili kuchangia hotuba ya Rais katika ufunguzi wa Bunge la 13 ya Jamhuri ya Kenya. Hii hotuba imesemekana na wachanganuzi kwamba ilikuwa fupi zaidi kati ya hotuba zote katika historia ya Kenya. Ningependa kusema ya kwamba hii hotuba ilikuwa fupi na ilikuwa nzuri. Sio lazima hotuba iwe ndefu ili iwe nzuri. Vitu vinaweza kuwa vifupi na vizuri. Bw. Spika wa Muda, hii hotuba ilikuwa ni ya kutupatia mwelekeo wa uongozi wa rais kwa kipindi cha miaka mitano hasa kuangazia mambo ya uchumi. Riwaza za pande zote mbili; Azimio la Umoja na Kenya Kwanza, zilikuwa zinaangazia mambo ya uchumi. Upande wa Azimio la Umoja ulikuwa unaangazia mambo ya mapinduzi ya uchumi na Kenya Kwanza ulikuwa unaangazia mambo ya kubadilisha uchumi kupitia mfumo wa makalio juu almaarufu bottom up. Kwa vile katika mashindano lazima kuwe na mshindi na mshinde, hii ruwaza ya"
}