GET /api/v0.1/hansard/entries/1201405/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1201405,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201405/?format=api",
    "text_counter": 485,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, Rais alianza kwa kupongeza viongozi waliochaguliwa. Kwa hivyo, ningepeda kuchukua fursa hii kuwashukuru wananchi wa Taita Taveta kwa kunichagua tena kwa awamu ya pili kwa sababu wanaamini uongozi wangu. Pia, nachukua fursa hii kuwapa kongole Maseneta wote waliochaguliwa na wananchi na vile vile wale walioteuliwa kuwakilisha vikundi tofauti. Vile vile, nampongeza Rais kwa kuchaguliwa kama Rais wa Jamhuri ya Kenya. Watu husema kuwa katika kila mashindano, lazima kuwe na mshindi na mshinde. Katika aya ya tatu, Rais alisema kwamba Serikali yake itashirikisha maeneo yote ya Kenya katika uongozi. Alipendekeza kuwe na Mawaziri 22. Hata hivyo, kuna baadhi ya maeneo ambayo hakuna Waziri hata mmoja aliyeteuliwa. Mfano ni Kaunti ya Taita Taveta. Kusema ukweli, hatuwezi kuwa na Mawaziri kutoka kila sehemu ya Kenya. Kuna Makatibu Wakuu na pia Chief Administrative Secretaries (CASs) ambao hawajachaguliwa. Tunasubiri mahakama kuamua iwapo ni sawa kuwa na CASs. Ikiwa"
}