GET /api/v0.1/hansard/entries/1201407/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1201407,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201407/?format=api",
    "text_counter": 487,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "hivyo, namwomba Rais aangazie maeneo ambayo yaliachwa nyuma katika uongozi kama vile Jimbo la Taita Taveta ndio angalau tuwe na Katibu Mkuu au hata CAS. Bw. Spika wa Muda, aya ya 21 inaangazia mambo ya kutoa ruzuku na pembejeo, haswa mbolea. Rais aliamuru bei ya mbolea kushuka kutoka Kshs6,500 hadi Kshs3,500. Namshukuru Rais kwa jambo hilo. Jinsi wengine walivyosema, hii si mara ya kwanza kwa Rais kushukisha bei ya mbolea. Mwaka wa 2008, akiwa Waziri wa Kilimo katika Serikali ya “Nusu Mkate”, alishukisha bei ya mbolea kutoka Kshs6,000 hadi Kshs2,400. Vile vile amefanya hivyo. Kushukisha bei ya mbolea pekee hakutasaidia kuhakikisha kuna food security . Kuna maeneo kama vile Kaunti ya Taita Taveta ambayo kando na kupata pembejeo, mambo kadha wa kadha yanafaa kufanyika ili kuhakikisha kwamba kuna chakula. Kuna maeneo kama vile Wundanyi na Werugamghange ambapo tukipata mvua vizuri, tulime na tupate mbolea, basi kutakuwa na mazao. Wananchi wa huko hawavuni kwa sababu ya shida za wanyamapori kama vile tumbili. Wananchi wa Wundanyi hawawezi kulima kwa sababu ya tumbili. Kando na pembejeo, Serikali pia inafaa kujua jinsi wakulima hao watalima. Wenyewe wana bidii ya kulima lakini chakula chao chote kinaliwa na nyani na tumbili. Njia gani zinaweza kutumika kulinda chakula cha wananchi hao dhidhi ya wanyamapori kama vile tumbili na nyani? Lazima kuwe na mikakati mwafaka ya kuhakikisha kwamba nyani na tumbili wameuawa au wafungiwe mahali ili wasifike kwenye mashamba yao. Hata ukiwapa mbolea watu wa maeneo ya chini kama vile Mwatate, Voi, Taveta na mengineyo ya Wundanyi kama vile Kishushe, hawawezi kulima kwa sababu hakuna maji. Wanategemea unyunyiziaji mashamba maji. Bw. Spika wa Muda, kando na kutoa mbolea ambayo imetolewa ruzuku, lazima kuwe na mpango mwafaka wa kuleta maji katika maeneo kame ya Kaunti ya Taita Taveta. Bw. Spika, kama unavyojua, Taita Taveta, kuna vyanzo vingi sana vya maji vinavyohitaji hela kidogo tu. Kwa mfano, kuna Ziwa la Challa, Ziwa la Jipe, Mzima Springs na Njoro Springs. Hivyo ni vyanzo vya maji ambavyo Serikali ikiwekeza pesa kidogo tu kama Kshs5 bilioni hadi Kshs10 bilioni, maeneo yote ya Mwatate na Voi yatapata Maji. Tukipata pamoja na ile mbolea ambayo imetolewa ruzuku, basi wananchi wataweza kulima na kupata chakula chao cha kutosha na hata chakula cha kuuzia Kenya nzima. Maeneo ya Taita Taveta ni maeneo yanayojulikana kuwa hayana ugonjwa katika mambo ya kufuga wanyama. Yale maeneo yakipewa maji na wananchi wapande nyasi, ni maeneo ambayo tunaweza kufuga ngómbe wengi na kupata wa kutosha Wakenya na pia kuuza nchi za ngámbo na pia kuleta ajira nyingi sana. Namshukuru Mheshimiwa Raisi kwa sababu katika aya ya ishirini na nane, ameongea mambo ya kutafuta pesa kwa kima cha Kshs900 bilioni kupitia mfumo wa Public Private Partnership (PPP), ama kutumia serikali na idara ambayo si ya serikali, ili kupata pesa ya kutosha ya kupata na kupeleka maji katika sehemu kame. Hilo naliunga mkono kwa sababu maeneo ambayo yana rotuba lakini hayana maji yanaeza kugeuzwa ili tunyunyizie mashamba maji na tuache ukulima wa kutegemea mvua. Ingawaje tumejaribu hili wakati mwengine maeneo ya Kilifi, kwenye mradi wa Galana Kulalu na haikufaulu. Lakini hata kama haikufaulu huko, hatuwezi kusema"
}