GET /api/v0.1/hansard/entries/1201409/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1201409,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201409/?format=api",
    "text_counter": 489,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "kwamba haiwezi faulu hata sasa. Kama Waisiraeli walifanya na wakafaulu, basi tuwalete huku watusaidie ili tuweze kufaulu. Katika mpango wa PPP, hii miaka mitano iliyopita tulikuwa tunasukuma mapendekezo tuliyokuwa nayo. Tuliyapeleka kwa PPP department kule Treasury ila hawakupitisha huo mradi wa Njoro Kubwa uliohitaji pesa kiwango cha Kshs6 billion na ulikuwa unalipiwa na sekta ambazo si za Serikali. Najua saa hizi saa hizi utaenda kupita, kwa sababu Raisi amesema watatumia hiyo mbinu ili kupata wafadhili wa kuleta maji kupitia mpango wa PPP, ili tupate maji ya kunyunyizia mashamba yetu. Katika maeneo haya kame, wananchi wanalima lakini hawawezi kuvuna kwa sababu ya kero la ndovu na wanyama pori. Ni vizuri serikali za kaunti, Serikali ya Kitaifa na Kenya Wildlife Service (KWS) washirikiane ili waweke nyaya za stima za kuzuia ndovu wasiingie katika maeneo ambayo wananchi wetu wanalima. Lingine ni kuhusu hii Kshs50 bilioni ambayo inaitwa Hustler Fund . Hii ndio itakayobadilisha uchumi wa Kenya. Kama kila Kaunti inaweza kupata Kshs1 billion ielekezwe kwenda kwa vijana, akina mama na walemavu, wapewe tender - Seneta wa Uasin Gishu ameongea vizuri sana kuhusu hii - wapewe pesa ya kufanya miradi na kaunti. Serikali ya Kitaifa au Treasury iangazie kwamba ile pesa imelipwa katika zile tender, basi wananchi wa chini ambao ni vijana na kina mama wanaoitwa hustler, wataweza kusaidika. Lakini tukifanya kama zile pesa zingine zilivyo, kwamba zinakopwa na kufanya biashara na Kaunti na Kaunti haziliwapi, wanakuwa na pending bills, basi huu mfumo wa pesa ya hustler bado hautasaidia wananchi wetu kujikuza kiuchumi. Jukumu letu kama Bunge ni kusaidia Serikali iliyoko kutengeneza sera, sheria na kanuni mwafaka za kusaidia hii hustler fund ifanye kazi vizuri kwa manufaa ya wananchi wetu. Hivi ndivyo tutapima Serikali yetu ya Kenya Kwanza kwa sababu haya ni mawazo yao wenyewe. Jambo lingine la muhimu ni kuhusu kufufua uchumi. Tumeona kwamba uchumi umelemaa hususan katika maswala ya utalii Kaunti za pwani. Watalii wengi waliokuwa wakuja pwani wameweza kuenda katika maeneo mengine kama Zanzibar ambao ni jirani."
}