GET /api/v0.1/hansard/entries/1201410/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1201410,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201410/?format=api",
"text_counter": 490,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Hii imesababishwa na kufungwa kwa viwanja vya ndege na mashirika ya ndege nchini. Kwa mfano, ukienda nchini Zanzibar kuna ndege zaidi ya kumi ambazo zinatoka nchi za kigeni kila siku. Zinaleta watalii katika nchi ile ilhali Mombasa Kaunti haina ndege hata moja na hiki ni kiwanja cha kiwango cha kimataifa. Miaka mitatu nyuma, kiwanja kile kilikarabatiwa na takriban shillingi billioni saba. Hata hivyo, hatujaona ndege zozote za kimatiafa zikishuka na kuleta watalii na kurahisisha usafiri baina ya Mombasa na miji miingine mikubwa ulimwenguni."
}